Sunday, 14 April 2019

Mwanafunzi adukua mtandao wa serikali na kujiajiri, Afrika Kusini


Mwanamme mmoja nchini Afrika Kusini anasakwa na polisi kwa madai ya kudukua data za serikali katika Sekta ya Afya kisha kujiajiri mwenyewe na kwamba amekuwa akipokea mshahara kuanzia mwezi Juni mwaka wa 2018.
Bright Chabota ambaye alisomea kozi ya uhandisi wa tarakilishi, Computer Engineering ni wa asili ya Zambia ila mamaye ni wa asili ya Zulu nchini Afrika Kusini. Inaarifiwa hakuwahi kwenda kazini ila amekuwa akipokea mshahara kila mwisho wa mwezi.
Kulingana na serikali, Chabota aligunduliwa baada ya kubainika kwamba hajakuwa akilipa kodi, vilevile ada za bima ya matibabu nchini humo.

Wazazi wake tayari wamehojiwa na wanasema kwamba mwanawe aliwaarifu kwamba alikuwa amepata kazi na kwamba alikuwa akilipwa Randi elfu saba kila mwisho wa mwezi kuanzia Juni mwaka wa 2018.
Kumbuka kwamba randi elfu saba za Afrika Kusini ni sawa na shilingi 1,161,408.21 za TANZANIA

No comments: