
Tanzania inatakiwa ije na programu nzuri zaidi ya miaka 10 ijayo itakayoiondoa hapa ilipo na kuipeleka mbali, lakini kama ni hivi lazima ichezee kichapo tu. Kabla ya mchezo huo, Rais wa TFF, Jamal Malinzi aliwatembelea wachezaji hao na kuwataka wafanye kila wawezalo kushinda, kwani aibu wanayoitoa si yao, ila yeye anaibeba kwa kiasi kikubwa. Malinzi pia aliwaahidi wachezaji hao kila mmoja Sh milioni 1 iwapo watashinda mchezo huo wa kwanza wa raundi ya kwanza Timu hizi zitarudiana wiki mbili zijazo. “Watu wanataka ushindi, matusi yote kwa TFF, huyo Malinzi anatukanwa kila sehemu. Nyinyi wenyewe mnatukanwa, mnapigwa mawe. Kwa kweli hali na mbaya. TFF tumejitahidi kuwafanyia kila kinachostahili na tutaendelea kuwafanyia, ni jukumu letu na hakuna siku tumewanyima, tungekuwa na posho zaidi, tungewapa. “Lakini sisi tunafanya mambo yetu nje ya uwanja, mkikanyaga uwanjani ni nyinyi, Bocco... kapaisha, Ndemla kapigwa chenga... kesho ni vita kubwa haijawahi kuonekana, Waganda mnawajua, (Nadir Haroub) Cannavaro mjitahidi kukimbizana nao, msicheze kama mpo ugenini, pambaneni kwa kujiamini, mpo nyumbani,” alisema Malinzi. Cannavaro aliahidi watajitahidi kulipigania taifa lao lakini mambo yalikuwa kinyume. Hii ni mechi ya tano mfululizo kwa Mart Nooij kufungwa ikiwemo iliyopita ya kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) walipofungwa 3-0 na Misri mwishoni mwa wiki mjini Alexandria. Kama Stars itaitoa Uganda itacheza na Sudan na mshindi wa mchezo huo moja kwa moja atafuzu CHAN 2016 nchini Rwanda.
No comments:
Post a Comment