Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Kati imeteketeza bidhaa
zisizofaa kwa matumizi ya binadamu zenye thamani ya Sh. milioni 20.
Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa kazi ya uteketezaji jana
mjini hapa, Kaimu Meneja wa TFDA Kanda ya Kati, Fredrick Luyangi,
alisema bidhaa zilizoteketezwa zina uzito wa tani 4.4.
Luyangi alisema bidhaa hizo ni dawa tani 0.44, chakula tani 3.08 na vipodozi uzito wa tani 0.93.
Aidha, TFDA imewaonya wafanyabiashara kuacha kuuza bidhaa
zisizofaa, zilizoisha muda wa matumizi na pia vipodozi vyenye viambata
vilivyopigwa marufuku baada ya kuonekana kuwa vina sumu.
"Wafanyabiashara wote wanatakiwa kuzingatia kanuni na sheria ili
wauze dawa, vyakula na vipodozi vinavyofaa kwa matumizi ya binadamu,"
alisema.
Aliongeza vilevile kuwa wananchi wanapaswa kuepuka matumizi ya
vyakula, dawa na vipodozi ambavyo vimeisha muda wake na ambavyo
havijasajiliwa nchini.
No comments:
Post a Comment