Sunday, 14 June 2015

Jeneza la Saddam Husen larudisha baada ya kuibiwa

Jeneza la Tareq Aziz lililodaiwa kupotea lapatikanaJeneza la Tareq Aziz lawasili katika mji mkuu wa Amman nchini Jordan

Mwili wa aliyekuwa kiongozi wa karibu wa Saddam Husein Tareq Aziz, umewasili katika mji mkuu wa Amman nchini Jordan.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa familia na baadhi vyanzo vya habari, jeneza la Tareq Aziz lilidaiwa kutoroshwa na kundi moja la watu waliojihami kwa silaha.
Serikali ya Iraq imekanusha madai hayo na kusema kwamba jeneza hilo lilisubirishwa Baghdad kwa muda kutokana na baadhi ya taratibu zilizokuwa zikifuatiliwa.
Waziri Mkuu wa Iraq Haydar Abadi, alitoa idhini ya kuwasilishwa kwa jeneza la Tareq Aziz kwa familia yake nchini Jordan pasi na kufanyiwa sherehe wala maandamano ya aina yoyote.
Tareq Aziz ambaye ni waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Iraq na aliyewahi kuhudumu kama naibu waziri mkuu wakati wa utawala wa Saddam Husein, alifikishwa hospitalini kutoka kwenye gereza alilofungwa na kupoteza maisha tarehe 5 mwezi Juni akiwa na umri wa miaka 79.

No comments: