Mfalme wa mwituni Simba ,atarejea Rwanda kwa mara ya kwanza tangu aangamie wakati wa mauaji ya kimbari mwaka wa 1994
Maafisa
wanaowalinda wanyama pori wa Rwanda, wanasema kuwa simba watarudi
nchini humo siku ya jumatatu kwa mara ya kwanza, tangu walipoangamizwa
baada ya mauaji ya kimbari,ya mwaka wa 1994.Simba wawili dume, na majike watano, wanasafirishwa kutoka mbuga ya wanyama ya Kwazulu Natal, Afrika Kusini, na Jumatatu watawasili Rwanda kwa ndege.
Wanyama hao watapelekwa katika mbuga ya taifa ya Akagera.
Maafisa wakuu huko Rwanda walisema, kurejeshwa tena kwa simba nchini Rwanda ,ni Kilele cha juhudi kubwa ya kuhifadhi mazingira katika mbuga hiyo na kwa taifa zima kwa jumla.
Simba waliokuwa humo walikimbia au kuuawa, huku watu wakijaribu kulinda mifugo yao na maisha yao.
No comments:
Post a Comment