Wasafarishaji
na wafanyabiashara wamesema hawawezi kukwepa kupandisha bei za bidhaa
na nauli kutokana na ongezeko la kodi ya mafuta ya Petrol na Disel
katika bajeti iliyosomwa na serikali bungeni ya mwaka 2015-2016 huku
wakitoa maoni ya nini kifanyike kuepuka bajeti kandamizi kwa wananchi.
Wakizungumza na ITV kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam
kiongozi wa chama cha wamiliki wa mabasi na msemaji wa chama cha
wamiliki wa malori wamesema licha ya bei ya mafuta kuongezwa gharama
lakini pia vipuri magari vimepanda bei baada ya dola kupanda kwani
bidhaa hizo wanauziwa kwa dola na kuongeza kuwa kwa bajeti hiyo bado
mwananchi wa kawaida ataendelea kuumia.
Kwa upande wa mwenyekiti wa umoja wa wafanyabiashara nchini Bw
Johnson Minja amesema walitegemea serikali ingepanua wigo wa kuongeza
idadi ya walipa kodi ikiwemo kurasimisha idadi kubwa ya biashara ambazo
halipiwi kodi pamoja na kuweka mkazo maeneo ya uzalishji ikiwa ni pamoja
na kuwabana wakwepa kodi badala ya kushughulika na maeneo yanayomgusa
mwananchi wa kipato cha chini.
Badhi ya wanasiasa nao wamezungumzia bajeti hiyo ambayo wamedai
kuwa wakati umefika kubuni vyanzo vipya vya mapato ambavyo vitampa
unafuu mwananchi hasa kwa kutilia mkazo maeneo ya utalii na madini,
lakini pia kuweka mfumo mzuri utakaowawezesha wakulima, wafugaji na
wavuvi kulipa kodi kwa mapato wanayopata.
No comments:
Post a Comment