Rais wa Shirikisho la Soka Duniani FIFA Sepp Blatter
aliyetangaza kujiuzulu anaweza kuomba kusalia katika wadhifa wake.
Taarifa hizo ni kwa mujibu wa gazeti moja nchini Uswisi likinukuu chanzo
kilicho karibu na Blatter ambacho hakikutaka jina lake litajwe .
Taarifa hizi zinatolewa katika kipindi kisichozidi wiki mbili baada ya
kiongozi huyo kutangaza kujiuzulu kuliongoza shirikisho hilo. Gazeti la
kila Jumapili la Uswisi Die Schweiz am Sonntag linasema Blatter amepokea
ujumbe wa kumuunga mkono kutoka kwa vyama vya soka vya Afrika na Asia,
vikimuomba afikirie upya uamuzi wake wa kujiuzulu. Chanzo hicho kimesema
Blatter amepokea vyema uungwaji mkono huo lakini bado hajafanya uamuzi
wa kuendelea kubakia katika ofisi. Hata hivyo FIFA haijaweza kujibu mara
moja barua pepe ya shirika la habari la Reuters kuhusu taarifa hizo.
No comments:
Post a Comment