Mahakama
ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC imeitaka Afrika Kusini kumkamata
rais wa Sudan Omar Al-Bashir ambaye anaripotiwa kusafiri kwenda nchini
humo kuhudhuria mkutano wa Muungano wa nchi za Afrika ambao unaanza leo
Jumapili.
Kwenye taarifa yake , ICC ilisema kuwa waranti mbili za
kumkamata Bashir bado ziko. Anatafutwa na mahakama ya uhalifu wa kivita
kuhusiana na uhalifu ulitokea katika jimbo la Darfur na anakabiliwa na
kesi inayohusiana na uhalifu wa kivita na mauaji ya halaiki.Kama mwanachama cha ICC, Afrika Kusini inastahli kumkamata Bashir ikiwa atasafiri kwenda nchin humo . Lakini Muungano wa Afrika umekataa kushirikiana na mahakama hiyo ya kimataifa ukisema kuwa ICC inawaonea viongozi wa Afrika.
No comments:
Post a Comment