Sunday 14 June 2015

Sijaona wakunioa asema Recho


NYOTA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Winfrida Josephat ‘Recho’ amesema bado hajampata mwanaume ambaye anaweza kumwita mume wake ndio maana hadi sasa yuko peke yake (singo).
Akizungumza Dar es Salaam jana, Recho alisema anaamini kuwa ni rahisi kwa msichana mrembo na staa kama yeye kuendelea kuwa peke yake na kwamba huo ni uamuzi wa mtu.
Alisema kwa sasa bado hana mwanaume aliyemchagua kwaajili ya kutafuta familia na kuilea wakiwa pamoja kama mume na mke.
“Bado nipo mwenyewe nafanya kazi, kwanza wanaume wapo na endapo atapatikana kila mtu atafahamu lakini kwasasa bado nipo mwenyewe natafuta maisha,” alisema.
Alisema sio kwamba hakuna wanaume wanaompenda, wapo lakini bado hajaona mwanaume ambaye anaamini atakuwa mzazi bora katika familia yake hapo baadaye.

No comments: