Monday 15 June 2015

Taifa stars yachapwa 3-0 na mafarao

Timu ya Taifa ya Tanzania jana Imeendeleza wimbi la kupoteza mechi Mfululizo chini ya kocha wao  Mdachi Mart Nooij

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, leo imepoteza mchezo wake wa kwanza kuwania kufuzu kwa fainali za AFCON mwaka 2017 baada ya kufungwa kwa mabao 3 – 0 na wenyeji Misri.
Taifa Stars ilicheza vizuri kipindi cha kwanza na hasa sehemu ya ulinzi ilifanya kazi ya ziada kuokoa mashambulizi ya washambuliaji wa timu ya Misri, na kupelekea kwenda mapumziko -0 – 0.
Kipindi cha pili Misri walifanya mabadiliko yaliyowapelekea kupata mabao hayo 3 ndani ya dakika 10, kupitia kwa Ramy Rabia(60), Basem Morsy(64) na Mohamed Salah (69).
Stars ilifanya mabadiliko ya kuwaingiza Frank Domayo, Saimon Msuva na Salim Mbdonde na kufanya shambulizi kadhaa langoni kwa Misri lakini mashambulzi hayo yaliokolewa na walinzi wa timu ya Misri.
Mara baada ya mchezo huo, Taifa Stars inaondoka leo Alexandria kuelekea Cairo ambapo itaondoka na shirika la ndege la Ethiopia saa 8 usiku na kufika jijini Dar es salaam jumanne saa 7 mchana.
Tanzania: Deogratias Munish, Shomari Kapombe, Oscar Joshua, Aggrey Morris/Salim Mbonde, Nadir Haroub, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto/Saimon Msuva, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samata, Amri Kiemba/Frank Domayo.
Misri: Ahmed El Shenawy, Ahmed Hegazy, Ramy Rabea, Mohamed Abd Elshafy, Hazem Emam, Mohamed Elneny, Ibrahim Salah, Mahmoud Abd Elmonem/Ramadan Soffiy, Mohamed Salah/Mostafa Ftahy, Doly Elgabay/Basem Morsy, Ahmed Hassan Meky.

No comments: