Mlinzi
wa klabu ya Paris St-Germain David Luiz amevishtumu vyombo vya habari
kwa kukosa heshima baada ya kukanusha madai kwamba yeye hajawahi
kushiriki katika tendo la ngono.
Ripoti hizo zilianza kusambaa
baada ya mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea mwenye umri wa miaka 28
kusema katika instagram kwamba yeye na mpenziwe ''wako tayari
kungojea''.Aliiambia BBC focus kwamba.''Dini yangu,ubaatizaji wangu,nafurahia.
Watu wanasema maneno kila mahala kuhusu iwepo mimi sijawahi fanya tendo la ngono.''Ukweli ni kwamba mimi nishawahi kushiriki katika tendo hilo''.
Aliongezea:Watu wengine katika vyombo vya habari hawaheshimu maisha ya watu.
Mimi ninawaheshimu wenzangu kwa hivyo sina bughudha ya aina yoyote.
No comments:
Post a Comment