Wednesday, 6 May 2015

Ligi ya Mabingwa: klabu tatu za Algeria katika kundi moja!

Kipa wa ES Setif, Sofiane Khedairia.Klabu za Algeria ikiwa ni pamoja na ES Setif, USM Alger na MC Eulma zimejikuta katika kundi moja na Al Merreikh kutoka Sudan la (B), katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa. TP Mazembe kutoka (DRC) katika Kundi A pamoja na Smouha (Misri), Tetouan (Morocco) na Al Hilal (Sudan).

Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limeamua kupanga ratiba ya michuano hiyo baada ya droo kupigwa kwa ajili ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa, leo Jumanne Mei 5 mwaka 2015 mjini Cairo. Kundi la Algeria ambalo lina asilimia 75 limeondolewa, kwani ES Setif, mabingwa wa Afrika, USM Alger na MC Eulma ziko pamoja na Al Merreikh kutoka (Sudan).
Itakumbukwa kwamba Algeria ni kwa mara ya kwanza katika historia yake, kuwa na wawakilishi watatu katika hatua hii ya mashindano.
Katika Kundi B, TP Mazembe imefanikiwa kuwekwa katika kundi moja na Smouha SC (Misri) pamoja na Moghreb Tetouan kutoka (Morocco) na Al Hilal (Sudan).

Hatua hii ya makundi itachukua muda wa siku sita. Klabu mbili kutoka kila kundi zitachuana katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali, michuano ambayo imepangwa kuchezwa tarehe (25 hadi 27 mwezi Septemba) na mmichuano ya marudiano imepangwa kuchezwa tarehe (02 hadi 4 mwezi Oktoba).
Kundi A linaundwa na Smouha SC (Misri), Moghreb Tetouan (Morocco), TP Mazembe (DRC), Al Hilal (Sudan).
Kundi B linaundwa na ES Setif (Algeria), USM Alger (Algeria), Al Merreikh (Sudan), na MC Eulma (Algeria)
Siku ya kwanza (Juni 26-28)
Siku ya pili (Julai 10-12)
Siku ya tatu (Julai 24-26)
Siku ya nne (Agosti 07-09)
Siku ya tano (Agosti 21-23 )
Siku ya sita (Septemba 11-13)

No comments: