Tuesday 26 May 2015

Chadema yasema njia sahihi ya kuiangusha CCM ni wananchi kujiandikisha kwa wingi kupiga kura

Chama cha Demokarasia na maendeleo Chadema kimesema njia sahihi ya kuindoa CCM madarakani ni wananchi kujitokeza kwa wingi na kujiandikisha katika daftrali la kupiga kura linaloendelea hivi sasa katika mikoa mbalimbali hapa nchini.
Kauli hiyo imetolewa na mwanasheria wa chama hicho.Tundu Lissu wakati alipokuwa akiwahutibiwa wananchi wa mji wa Bariadi na Meatu mkoani Simiyu ikiwa ni sehemu ya ziara ya viongozi wa chama hicho wanayofanya nchi nzima ya kuhamisha zoezi hilo.
 
Amewataka wananchi wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi ifikapo tarehe 2,mwezi wa sita katika vituo na kujiandikisha ili weweze kupata haki ya kupiga kura mwezi wa kumi mwaka huu kwani ndiyo njia pekee ya kuiondoa serikali ya chama cha mapinduzi madarakani.
 
Aidha amesema yeye na wabunge wenzake wa chama hicho wameamua kuondoka bungeni na kuzunguka nchi nzima kwa ajili ya kutoa elimu hiyo ili wananchi waweze kujiandikisha baada ya kugundua kuwa zoezi hilo limegubikwa na ujanja mwingi

No comments: