Mchezo
wa kwanza wa nusu fainali za Kombe la Mabingwa barani Ulaya kati ya
Juventus ya Italia dhidi ya Real Madrid ya Hispania umefanyika Jumanne
usiku kwa Juve kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Juventus wenyeji
wa pambano hilo walipata bao lao la kwanza katika dakika ya 8 ya mchezo
kupitia kwa Alvaro Morata. Hata hivyo Cristiano Ronaldo alisawazisha
katika dakika ya 27. Matokeo yaliyodumu hadi kipindi cha kwanza
kinamalizika.Juventus walipata goli tena katika dakika ya 57, kutokana na mpira wa adhabu ya penalti, ambapo Carlos Tevez aliifungia timu yake. Hadi kipenga cha mwisho, Juventus 2, Real Madrid mabingwa watetezi 1. Timu hizo zitarudiana tarehe 13 Mei katika uwanja wa Bernabeu, mjini Madrid.
Katika pambano lingine la nusu fainali za Kombe la UEFA, timu nyingine ya Hispania, Barcelona wanawaalika Bayern Munich ya Ujerumani Jumatano usiku katika uwanja wa Nou Camp. Barcelona itakuwa na kibarua kigumu kuwaangusha Bayern ambayo kwa sasa inafundishwa na kocha wake wa zamani Pep Guardiola.
No comments:
Post a Comment