Watu watatu wameuawa na wengine zaidi ya ishirini wamejeruhiwa katika milipuko mitatu ya guruneti ziliyorushwa kwenye kituo cha mabasi jijini kati Bujumbura leo Ijumaa jioni. Waliondesha mashambulizi hayo hawajulikani. Idadi hiyo ya watu 3 waliopoteza maisha huenda ikaongezeka.
Wakati huo huo maandamano yameendelea leo Ijumaa katika wilaya
mbalimbali za jiji la Bujumbura. Maandamano hayo yameendelea wakati
ambapo mkurugenzi na mmiliki wa kituo cha redio na telivisheni
Rennaissance Fm, Innocent Mohozi amesikilizwa kwenye Ofisi ya mashataka.
Rennaissance Fm ni moja ya vyombo vya habari binafsi vilivyoshambuliwa na kuchomwa moto wakati wa jaribio la mapinduzi, juma moja lililopita.
Innocent Muhozi amesikilizwa kwa muda wa masaa 4, lakini aliruhusiwa kurejea nyumbani kwake. Afisaa wa mashtaka amemsikiliza mkurugenzi huyo katika lengo la kuendesha uchunguzi kuhusu jaribio la mapinduzi.
Ofisi ya mashtaka imemuhoji mkurugenzi wa kituo cha redio na televisheni Rennaissance Fm kuhusu kurushwa hewani kwa tangazo la jenerali Godefroid Niyombare la mapinduzi ya serikali, Jumatano wiki iliyopita.
Mpaka hatua hii Innocent Muhozi ana imani kuwa hatorudi kufuatiliwa na vyombo vya sheria, lakini ana hofu kuwa huenda vyombo vya sheria vikashinikizwa kutumia mbinu nyingine.
“ Uchunguzi umeanzishwa, nina imani kuwa sintorudi kufuatiliwa, kwani tulitekeleza kazi yetu ya uandishi wa habari ”, amesema Innocent Muhozi.
Mpaka sasa Innocent Muhozi hajaikimbia nchi yake wala kuingia mafichoni kama wakurugenzi wa vituo vya redio binafsi vingine.
Mkurugenzi huyo wa kituo cha redio na runinga binafsi Rennaissance Fm ameeleza kuwa polisi ndio iliyovamia na kuchoma moto majengo ya kituo chake cha redio na runinga

No comments:
Post a Comment