Msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje wa Marekani Marie
Harf, amesema nchi hiyo imesimamisha kwa muda mafunzo inayotoa kwa
wanajeshi wa Burundi kwa ajili ya operesheni za kulinda amani, kutokana
na wasiwasi kuwa mgogoro wa kisiasa nchini Burundi huenda ukaathiri
uwezo wa wanajeshi wake wa kushiriki katika operesheni hizo. Uamuzi wa
rais Pierre Nkurunziza mwezi uliopita wa kutaka kuwania muhula wa tatu
madarakani, umesababisha maandamano yaliojaa vurugu, jaribio la
kuipindua serikali na kusababisha maelfu ya warundi kukimbilia nchi
jirani. Kulingana na Ikulu ya Marekani tangu mwaka wa 2005 kupitia
mpango wa kutoa mafunzo na kuwasaidia wanajeshi wa Africa ACOTA,
Marekani imeshatoa mafunzo hayo kwa wanajeshi wa kulinda amani zaidi
ya 248,000 katika nchi 25 barani Afrika kabla ya kupelekwa katika kikosi
cha Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika katika operesheni za kulinda
amani.
No comments:
Post a Comment