Monday 25 May 2015

Basi la kampuni ya Super Feo la pinduka na kuua watu 3 na wengine 28 kujeruhiwa

Watu 3 wamekufa papo hapo na wengine 28 kujeruhiwa baada ya basi la kampuni ya Super Feo walilokuwa wakisafiria kutoka jijini Mbeya kwenda Songea mkoani Ruvuma kupinduka na kutumbukia mtoni katika kijiji cha Shamwenga kata ya Inyara wilayani Mbeya.
Ajali hiyo imetokea baada ya basi la kampuni ya Super Feo likiwa kwenye mwendo mkali kujaribu kulipita lori lililokuwa mbele yake, lakini kabla halijafanikiwa kulipita kwa mbele likatokea lori la mafuta, hali ambayo ikasababisha dereva wa basi kulikwepa kwa upande wa kulia, lakini akashindwa kulimudu na ndipo lilipopoteza mwelekeo na kutumbukia mtoni.
 
Daktari wa zamu katika hospitali ya rufaa Mbeya, Dk Lathan Mwakyusa amethibitisha kupokea miili ya watu watatu pamoja na majeruhi 28 wanaotokana na ajali hiyo.
 
Kwa upande wake afisa mfawidhi wa Sumatra mkoa wa Mbeya, Denis Daudi amesikitishwa na ajali hiyo na kuwataka madereva kuongeza umakini wawapo barabarani ili kuepusha ajali zinazoweza kuzuilika.

No comments: