Friday 1 May 2015

John Terry aingia kwenye rekodi EPL

CDyrMRcWgAET2ps
NAHODHA wa Chelsea, John Terry jana usiku amefunga goli moja kwa njia ya kichwa katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Leicester City.
Terry aliifungia Chelsea na kuufanya ubao usomeke 2-1 katika uwanja wa King Power akimalizia mpira wa kona dakika ya 79.
Kutokana na goli hilo, John Terry amefikisha magoli 38 katika maisha yake ya soka na kuungana na gwiji wa Everton David Unworth ambaye alifunga magoli hayo na kuwa beki aliyefunga magoli mengi zaidi ligi kuu England.
 David Unsworth kwasasa ni kocha wa timu ya vijana umri chini ya miaka 21 ya Everton.
Rekodi hiyo ya Terry haijavuka mipaka ya England, mtandao wa Opta umeandaa jedwali zuri siku ambayo Real Madrid ilishinda 3-1 dhidi ya Malaga ligi kuu ya Hispania, La Liga.
Real Madrid walishinda mechi hiyo huku beki wake Sergio Ramos akifunga goli kwa njia ya kichwa akimalizia mpira wa adhabu wa Cristiano Ronaldo na goli hilo lilimfanya awe beki huyo mwenye miaka 29 kufikisha goli la 40 katika maisha yake ya soka.
Sergio Ramos ndiye beki anayeongoza kufunga magoli mengi zaidi katika ligi 5 barani ulaya katika muongo uliopita.
Angalia jedwali chini

No comments: