Sunday, 31 May 2015

Barcelona bingwa mpya Copa del Rey

Messi ang’aa katika fainali; Barcelona yabeba Copa del ReyNyota wa Barcelona Lionel Messi alifunga bao la kukumbukwa katika fainali waliyowalaza Athletic Bilbao kwa magoli 3 kwa 1.

Lionel Messi aliongoza timu yake ya Barcelona kufikia kombe la Copa del Rey kwa mara ya 27 baada ya kushiriki katika fainali 38. Messi alitangulia kufunga bao la kwanza katika dakika ya 20 baada ya kuwapiga chenga walinzi 4 wa Athletic Bilbao na kufyatua kombora lililomwacha hoi mlinda lango.
Neymar alifunga la pili katika dakika ya 37 baada ya kuandalia lango wazi na Suarez.
Messi alirejea tena na bao la tatu katika dakika ya 74 na kumaliza kazi yake katika fainali hiyo.
Athletic Bilbao walipata bao la kufuta machozi katika dakika ya 80 kupitia mshambuliaji wao Inaki Williams.
Ushirikiano wa Messi, Suarez na Neymar maarufu kama MSN umevunja rekodi ya Ronaldo, Benzema na Higuain ya jumla ya mabao 118 katika msimu mmoja, baada ya kufunga jumla ya mabao 120 kufikia sasa.
Post a Comment