Waziri Mkuu wa Togo Kwesi Seleagodji Ahoomey-Zunu na serikali
yake walijiuzulu hapo jana Ijumaa, hatua iliotarajiwa baada ya Rais wa
nchi hiyo Faure Gnassingbe kushinda uchaguzi mwezi uliopita na hivyo
kuendeleza takriban miaka 50 ya utawala wa familia yake. Tarehe nne
mwezi huu, rais Gnassingbe aliapishwa rasmi kuchukua uongozi wa muhula
wake wa nne baada ya kushinda kwa asilimia 59 ya kura katika nchi hiyo
ya Afrika Magharibi. Aidha rais Gnassingbe alimshukuru Waziri Mkuu na
serikali yake kwa kuitumikia nchi akikubali kwamba kujiuzulu kwao
kunaendana na utaratibu wa nchi hiyo. Hata hivyo haijawa wazi iwapo
baadhi ya mawaziri waliojiuzulu watapewa nyadhifa za uongozi katika
serikali mpya.
No comments:
Post a Comment