Thursday 21 May 2015

Wafuasi wa chadema mkoani morogoro watawanyishwa kwa mabumu ya Machozi


Wafuasi wa CHADEMA watawanywa na Polisi Morogoro
Wafuasi wa chama cha maendeleo na Demokrasia CHADEMA wametawanywa na Polisi katika vurugu za kushangilia kuachiliwa kwa viongozi wao wapatao 11ambao walikuwa wanashikiliwa katika kituo kikuu cha polisi mkoani MOROGORO

Viongozi hao wameshikiliwa baada ya kushiriki katika shughuli ya kuwaapisha vijana takribani 150 wa kikundi cha Red Brigade ambao kwa mujibu wa chama hicho wanaandaliwa kwa ajili ya kulinda kura katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika octoba mwaka huu.

Watu walioathirika na mabomu ya machozi ni pamoja na mwanafunzi mmoja aliyeumia mguuni.

Na katika hatua nyingine, kundi lingine la uhalifu likiwa na watuhumiwa 12 limefikishwa katika mahakama ya mkoa wa morogoro na kusomewa mashitaka na mawakili wa Serikali Sundey, Hyera na Edga Bautulaki mbele ya Hakimu mkazi Agripina Kimanzi huku Hakimu huyo akiiahirisha kesi hiyo hadi Juni 5 mwaka huu kutokana na upelelezi kutokamilika .

Watu hao ambao walikamatwa katika misitu ya udzungwa baada ya mmoja wao kulipua bomu lililojeruhi watu 6 waliokuwa katika sherehe za may mosi katika kijiji cha Msolwa wilayani kilombero, wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama na kutenda kosa kinyume na sheria ya kupambana na makosa ya ugaidi.

Makosa mengine ni ya uchokozi wa kivita kujiandaa kuvamia kituo cha polisi na kujaribu kuua, ambapo hawakutakiwa kujibu chochote kwa vile mahakama hiyo haina mamlaka za kusikiliza kesi za aina hiyo

No comments: