Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benardb Membe. |
Habari za uhakika zilizopatikana jana Jijini Dar
es Salaam, zilieleza kuwa Watanzania hao, walirejea nchini jana alfajiri
na kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ndege ya
Shirika la Precision Air.
Hata hivyo, jitihada za kumpata Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe hazikuzaa matunda lakini
Naibu wake, Mahadhi Juma Maalim alithibitisha habari hizo.
“Ni kweli tumewarejesha Watanzania 26 waliwasili
leo (jana) asubuhi kutoka Afrika Kusini na hii ilikuwa ni ahadi ya
Serikali siku zote tunajali usalama wa raia wetu popote walipo,” alisema
Maalim.
Hivi karibuni, Waziri Membe alisema kuwa Serikali
ilikuwa na mpango wa kuwarudisha Watanzania hao baada ya kutokea
machafuko hayo kwa wenyeji kuwapiga na kuwaua wageni kwa kile walichodai
‘kuwaminya’ kwenye ajira zao.
Habari zaidi zilisema Watanzania hao walisafiri
kwa ndege kutoka Durban juzi usiku hadi Pretoria na usiku huo huo, wote
wakafanikiwa kupata nafasi kwenye ndege ya Precision na kurejea nchini
jana.
Wiki iliyopita, Membe alisema Watanzania 23
waliokuwa wamewekwa kwenye kambi maalumu ya Isipingo nchini Afrika
Kusini ili kupewa ulinzi kutokana na mashambulizi yanayofanywa na
wazawa.
Miongoni mwa Watanzania hao, 21 walikuwa
wameridhia kurejea nyumbani na wanatarajia kuwasili nchini muda wowote
lakini wengine wawili waliomba kuendelea kubaki nchini humo.
Membe alitumia mkutano huo kukanusha taarifa kuwa
wapo Watanzania waliofariki nchini humo kutokana na vurugu hizo akisema
watanzania waliofariki, walikufa kwa sababu mbalimbali.
Hata hivyo taarifa hizo zimekuwa zikipingwa
kupitia baadhi ya Redio na mitandao ya kijamii hapa nchini, huku Redio
moja ikimkariri mtanzania mmoja akidai alishuhudia watanzania wanne
wakifa
No comments:
Post a Comment