Akizungumza na waandishi wa habari mtu wa karibu na askari
hao amesema kuwa chanzo cha ugomvi wa askari hao ni wivu wa mapenzi ambapo
marehemu pamoja na mtuhumiwa ambaye ametambulika kwa jina la Faustine Masanja
wameona nyumba moja.
Amedai marehemu alipofika asubuhi kazini ndipo mtuhumiwa
Masanja alimpiga mwenzake risasi ya kichwa na alipokimbizwa katika hospitali ya
Mkoa Mount Meru alifariki dunia.
ASKARI magereza Faustine Masanja amemuua askari mwenzake
Ombeni Mwakiyani kwa kumpiga risasi kichwani.
Kamanda wa mkoani hapa, Charles Mkumbo amethibitisha kutokea
kwa tukio hilo lililotokea leo majira ya asubuhi wakati wakiwa kazini kwenye
gereza la mkoa la Kisongo.
Mmoja wa mashuhuda tukio hilo ambaye hakuwa tayari jina lake
kuandikwa alisema kuwa askari Masanja alimpiga risasi mwenzake wakiwa wanawapakia
mahabusu kwenye gari kwa ajili ya kuwapeleka kwenye mahakama mbalimbali za
mkoani hapa kwa ajili ya kusikiliza kesi zao.
"Masanja alikuja akampiga Ombeni risasi ya kichwa kwa
nyuma ikatokea usoni alipomaliza akatupa silaha chini akasema sikimbii
nikamateni kwa kuwa najua nimeua," alisema shuhuda huyo.
Hata hivyo baadhi ya askari magereza ambao hawakuwa tayari
majina yao kuandikwa walidai kuwa Ombeni na Masanja wake zao ni ndugu hivyo
kuna uwezekano kulikuwa na mgogoro wa kifamilia.
SOURCE: http://www.habaritanzaniagracemacha.com/
No comments:
Post a Comment