Wednesday, 13 December 2017

FAMILIA YA BEN SAANANE YA ANDIKA HAYA KUKUMBUKA SIKU YA KUZALIWA KWA BEN SAANANE

Ni mwaka mmoja na siku kadhaa tangia Ben Saanane atoweke/atoweshwe katika mazingira tatanishi.
Leo Ben, anamitiza miaka kadhaa tangia kuzaliwa kwake. Happy beloved birthday bro, hero and comrade!

Naelewa namna Baba, Mama, dada, kaka na ndugu zako wanavyo jisikia, ulikuwa kaka mkubwa, lango la familia, tegemeo, ulikuwa sehemu ya furaha ya familia, Leo walio kulea wanaumia, walitamani siku ya leo mshereheke siku hii pamoja, ila imekuwa tofauti, siku imekuwa ya mawazo na mateso kuliko tegemeo.
Masonokeno na Maumivu yao tumeyaishi, machozi katika mioyo yao hayakuwahi kauka, furaha yao imekuwa ya msimu, kila wakijaribu kupata furaha, kukosenaka kwako kunaondosha
furaha yao. Hakika furaha yetu itaendelea kuwa ya msimu, mpaka nyakati zile tutapo jua nini hatima yako. Uchungu tunao uishi ungepimika ungekuwa mzito kuliko mchaga wa baharini.
Angalau ingekuwa msiba tungesha omboleza yakaisha ila kwa namna ulivyo toweshwa, mioyo yetu inazidi kuchoka.
Wenye viburi vya uzima wanatunyanyasa, baba na mama nao wanaona giza, wanaumia marafiki na ndugu zako hali zao haziyumkiniki, hawaoni tumaini, Ni kipindi kigumu katika historia ya familia ya mzee Focus.

Ila katika yote, hatutakata tamaa, tupiga moyo konde, hata maandiko yanasema "duniani Kuna dhiki kubwa, ila jipeni moyo " Tutakaza moyo, tunaye MUNGU, yamkini ndiye aliye yaruhusu haya.

#Happybirthday
#WeMissYouBenSaanane

Happy beloved birthday, Ben Saanane.


Ndimi, Noel Shao
Post a Comment