Monday, 17 July 2017

TETESI ZA USAJILI LEO TAREHE 17/7/2017

Kulingana na gazeti la Sky Sports Klabu ya chelsea inataka kukamilisha dili la kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang , katika harakati hizo chelsea imeongeza dau lake kutoka paundi milion 65 hadi kufikia paundi ilion 70 kuhakikisha wanapata saini ya mchezaji huyo baada ya kumkosa Romeu Lukaku aliyetua Man U .


Klabu ya Mzee wenger imepania kumsajili beki wa Southampton Virgil van Dijk kwa dau la paundi milion 40 ili kujiimarisha kuelekea msimu ujao hata hivyo mzee wenger amepania pia kumsajili kiungo mshambuliaji wa Celtic Moussa Dembele kuziba nafasi ya Sanchez ambae bado mwafaka wake wa kubaki Arsenal uko matatani ( Daily Express ).

 Arsenal  imeweka ofa ya kumlipa Alex Sanchez £275,000 kwa week ili aendelee kubaki katika klabu hiyo yenye maskani yake mjini Landan ,lakini hata hivyo Sanchez alinukuliwa akisema anatamani kucheza champion League msimu ujao , Sanchez anafuatiliwa karibu sana na Man City pamoja na chelsea.

 Mshambuliaji wa Man city Sergio Aguero anakaribia Kutua katika klabu ya Chelsea muda wowote kwanzia sasa , makubaliana ya kumuuza mchezaji huyo kwa chelsea yamepata baraka zote tayari kwa kocha wa man city Pep Guardiola ( linaripoti gazeti la AS  journalist Manu Sainz).

Arsenal imegeukia upande wa Real Madrid ukimtaka mshambuliaji wa timu hiyo ambaye kawekwa sokoni na klabu hiyo ya real madrid Alvaro Morata, kocha wa Arsenal anaamini Morata atakuwa mridhi sahihi wa Alex sanchez ambaye haifahamiki kama atabaki Arsenal , Wenger anaamini kuwa Morata alaleta Muunganiko safi atakaposhirikiana na Alexandre Lacazette ambaye alisajiliwa hivi karibuni , Mzee wenger anakabiliana vikali na klabu za Ac Milan na Chelsea ambazo zinammezea mate mchezaji huyo pia (Don Balon .).


Post a Comment