Klabu ya Chelsea iliyo na maskani yake jiji la London imetuma ofa ya paund million 65 kwaajili ya kumsajili mshmbuliaji wa Borusia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang raia wa Gaboni.
Meneja wa Chelsea Antoni Conte ametuma ofa hiyo baada ya
kukosa saini ya aliyekuwa mchezaji wa Everton Romeo Lukaku ambaye sasa
amejiunga na mahasimu wao Manchester United jumatatu ya wiki hii. Mpango wa
kumsajili mshambuliaji huyo uekuja baada ya Chelsea chini ya meneja wake Conte
kuonekana hana mpango na Diego Costa kwa msimu ujao ,Kwa Upande wa Dortmund wamefungua milango kwa mchezaji huyo
kuuzwa , ripoti kutoka gazeti la “The Sun ” zineleza kuwa Pierre-Emerick
Aubameyang anatamani sana kucheza ligi ya Uingereza. Aubemeyang aliibuka
mpachikaji bora wa magoli katika ligi ya ujerumani msimu wa 2016/17, PSG na AC MILLAN pia zinafuatilia saini ya mchezaji huo kwa
karibu zaidi

Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane ametangaza kuachana na
mpango wake wa kutaka kumsajili kiungo wa Monaco Kylian Mbappe kutokana na ada
kubwa ya uhamisho inayoitajika na Monaco hivyo ameeleza kuwa atamshawishi
Mwenyekiti wa klabu hiyo Perez ili kukika nguvu zao kuipata saini ya Mchezaji
wa Chelsea Eden Hazard , akihojiwa na jarida laDiario Gol la nchini Uhispania
ZInedine ameeleza kuwa anaamini watatumia uhaisho wa Morata kwenda Chelsea kama
Chambo ya Kumpata Hazard

Klabu ya Man U licha ya kutishia kumwacha Mshambuliaji wake Zlatan
Ibrahimovic inatarajia kumwongezea mshambuliaji huyo mkataba wa muda mfupi
kutokana na kuonekana afya yake imeimarika kiasi cha kuweza kurudi uwanjani ,
hata hivyo Zlatan Ibrahimovic alikwisha mkabidhi romeu Lukaku namba ya jezi
yake.

Klabu ya Portsmouth iemsajili Golikipa kinda wa Totenham Luke
McGee (17), Luke alikuwa akichezea klabu ya daraja la kwanza Peterborough ambako
alionyesha mawanikio makubwa na kujitwalia tuzo ya mchezaji bora wa mwaka
katika ligi hiyo.
No comments:
Post a Comment