Sunday, 28 May 2017

Tetesi za Usajili Uingereza leoMshambuliaji wa Atletical Madrid aliyehusishwa kwa mda mrefu kuhamia Klabu ya Manchester United Antoine Griezman amewakatisha tamaa mashabiki wa man u baada ya kuandika katika akaunti yake ya twitter kuwa bado anafurahia kubaki A.Madrid na taarifa zinazomhusisha na kutaka kuhama ni za uongo zipuuzwe.

Mshambuliaji wa Chelsea na nchezaji wa timu ya taifa ya Ghana Christin Atsu aliyekwa akikipiga kwa Mkopo katika club ya Newcastle inayofundishwa na kocha wa zaman wa Mabingwa wa Uingereza kwa sasa Chelsea Rafael Benitez amekamilisha uhamisho wake wa moja kwa moja utakaombakisha katika kla
bu hiyo kwa ada ya uhamisho wa £6 million.

Manchester city wamewapiku jirani zao Manchester United kwa kumfanikisha kupata saini ya mchezaji wa Monaco Bernardo Silva kwa kiwango cha £43million . Huku klabu ya napoli ikifanikiwa kumbakiza mchezaji wake mahiri Dries Mertens ambaye mkataba wake ulikuwa unakaribia kufika kikomo , Dries Mertens ameingia mkataba mpya na klabu yake hadi 2022.
Mshambuliaji hatari wa Borussia Dortmund Aubameyang ameweka wazi kuwa anatamani kubadili mazingira na anatamani kufana kazi na klabu nyingine tofauti na Borussia Dortmund hata hivyo timu za ligi kuu nchini uingereza kama vile Chelsea zinamvizia mshambuliaji huyo hatari , chelsea chini ya meneja wake Conte inamwinda kinda huyo ili kuziba nafasi ya Diego Costa anaetimkia China msimu ujao na kuungana na wachezaji wenzake wa zaman kama Oscar , Ramirez na Dembaba.
Klabu ya Monaco ya nchini Ufaransa imeingia kwenye vita kali na klub ya newcastal katika kuwania saini   ya mshambuliaji wa Chelsea Michy Batshuayi.

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp anamtolea macho mchezaji wa kimataifa wa Ujermani na klabu ya Borussia Dortmund Mario Gotze ili kuziba pengo la mshambuliaji wake Philippe Coutinho
anaetazamiwa kujiunga na miamba wa soka nchini Uhispania Barcelona.

Katika hali ya sintofahamu wamiliki wa Arsenal juzi walikuwa wamemwahidi kocha wa Arsenal arsen wenger kuwa atapatiwa mkataba wa miaka miwili endapo watapata matokeo mazuri dhidi ya chelsea katika fainali ya kombe la FA , hata hivyo Wenger haku chezea bahati hiyo alifanikiwa kutwaa kombe la FA kwa kuwachapa Chelsea 2-1 , hivyo inatazamiwa wenger akaongezewa mkataba wa miaka miwili

No comments: