Aliyekuwa rais wa Tanzania Mh. Dr. Jakaya
Mrisho Kikwete ameteuliwa kuhudumu katika baraza kuu la wakimbizi
duniani WRC, ambalo ni kundi huru la viongozi na wavumbuzi wanaolenga
kubuni mbinu mpya za kutatua mizozo ya wakimbizi.
Kulingana na
gazeti la The Citizen nchini Tanzania, taarifa kwa vyombo vya habari
ilimtaja Bwana Kikwete kuwa mwenyekiti mwenza wa baraza hilo lililopo
chini ya uenyekiti wa waziri wa maswala ya kigeni nchini Canada Lloyd
Axworthy.
Gazeti hilo limesema kuwa Hina Jinali kutoka Pakistan na
Rita Sussmith kutoka Ujerumani watafanya kazi pamoja na bwana Kikwete
kama wenyekiti wenza huku Paul Heinbecker akichaguliwa kama naibu huku
naye Fen Hamson akihudumu kama mkurugenzi.
Taarifa hiyo imesema kuwa miongoni mwa mengine, baraza hilo
litatoa ushauri wa marekebisho na uvumbuzi ili kuimarisha mfumo wote wa
wakimbizi duniani.
Baraza hilo litaleta mabadiliko ili kusaidia
kuhakikisha kuwa ushirikiano wa kimataifa kwa wakimbizi unaeleweka,
unafanyika kwa njia ya usawa na haki, ilisema taarifa hiyo.
Baraza hilo pia litashirikisha madiwani 17 wa mabaraza.
No comments:
Post a Comment