Wednesday, 27 September 2017

Zanzibar na Uingereza ndio nchi pekee zilizopogana vita kwa muda Mfupi , dakika 40

Unaambiwa ukishangaa ya Musa utaona ya firauni, na siku hizi watu wanasema akili za mtu anazijua mwenyewe. Ili kudhibitisha hayo najaribu kukuletea simulizi hizi za kweli zilizotokea nyakati tofauti tofauti katika uso wa dunia. Siku zote migogoro huwa inatokea katika maisha ya binadamu na kunakuwa na sababu za kimasilahi kusababisha migogoro hio, wakati mwingine kumekua na migogoro ambayo mantiki za kimasilahi hazionekani, nakusababisha watu au pande mbili kwenda mbali Zaidi kiasi cha kutanagaza vita. Zifutazo ni vita vilivyo wahi kutokea kayika historia ya dunia na kuonekana za ajabu sana kulingana na sababu, muda au mbinu zilizotimika.

  1. VITA YA MUDA MFUPI ZAIDI DUNIANI.
hii ni vita kati ya uingereza na Zanzibar ambayo ilipigwa mwaka 1896, agost tarehe 27, ambapo vita hio ilipigwa kwa takribani dakika 40 tu, na Zaidi ya wanajeshi 500 wa zanzibar walijeruhiwa wakati mmoja tu wa upande wa Uingereza ndie aliejeruhiwa na sababu ya vita hio ilikua ni swala la mrithi atakae chukua madaraka baada ya sultan Hamad bin Thuwani ambapo sultan Hamad bin barghash alichukua madaraka kimabavu, kinyume na makubaliano ya mkataba uliopitishwa mwaka 1886 kati ya uingereza na Zanzibar kwamba mirthi wa kiti hicho lazima apitishwe na kukubaliwa na baraza la Uingereza. Hii ilisababisha mgogoro ambapo sultan barghash alipewa mda wakuachia madaraka kwa hiari lakini badala yake alikaidi na kupanga kikosi cha askari ilikumlinda. Jeshi la uingereza lilipanga vita na kuanza mashambulizi saa 3 na dakika 2 asubuhi na kutangaza ushindi saa 3 na dakika 40.

Pamoja na rekodi hii iliyowekwa kati ya Zanzibar na nchi ya Uingereza zipo rekodi nyingine mbalimbali zilizowekwa na nchi nyingine katika maswala ya vita
  1. VITA YA KILEVI MOLDOVA,
hii ni vita iliopigwa huko Moldova, baada ya ngome ya urusi kuanguka ma kuvunjika katika nchi ndogondogo, Moldova nayo ilikua moja ya nchi zilizotokea kama matokeo ya anguko hilo, tatizo likatokea pale wananchi wa Moldova walipo gawanyika katika makundi mawili kundi moja likiwa linataka Moldova ijiunge au ishirikiane na Romania na wengine ambao walikua wachache Zaidi, takribani theluthi moja ya idadi ya watu kutaka kushirikiana au kujiunga na  Ukraine au urusi yenyewe. Hivyo ndani ya nchi hio moja kukawa na watu wa Moldova na wengine wa Transdniestria na kuanza mapigano. Cha ajabu ni kwamba hawa watu walikua wanakutana usiku na kunywapombe pamoja huku wakipiga soga asubuhi kila mtu anaenda kambini kwake kuchukua silaha na mapigano yanaendelea, hivyo vuta hii iliitwa vita ya walevi.
  1. VITA YA MIAKA 335 BILA MAJERUHI
Kuanzia 1651 watawala wa uholanzi na wale wa visiwa vya Scilly vilivyopo kusini magharibi mwa Uingereza, wlitangaza vita ambavyo vilidumu mpaka mwaka 1986, japo kwa majibizano tu uhasama mkubwa, bila kutumia silaha lakini pia bila kupatikana kwa suluhisho, katika vita hio ya miaka 335 hakuna mtu aliefariki au kupata majeraha. Hivyo basi hii ni vita iliodumu kwa miaka mingi Zaidi duniani bila kusababisha vifo au majeraha. Vita hii iliisha mwaka 1986 baada ya kusainiwa kwa mkataba wa Amani.
  1. VITA YA MPIRA(FOOTBALL WAR)
Kwa kiingereza vita hii inafahamika kama football war, Honduras na El Savador zilikua katika sintofaham kwa muda mrefu na uhusiono uliogubikwa na mashaka pamoja na ujirani wa masimango kati ya nchi hizo mbili. Michezo inasemekana kuwa ni kichocheo cha urafiki lakini vita kati ya mahasimu hawa wa wili ilitokea baada ya mtifuano katika uwanja wa mpira wa miguu kati ya timu za mataifa hayo mawili, mchuano wa kufuzu kushiriki mashindani ya kombe la dunia mwaka 1970. Ugomvi wa uwanjani katika mchezo wa marudiano ulisababisha nchi hizi mbili zikaingia katika vita iliodumu kwa takribani masaa 100, mda ambao pia unaweza kuwa mfupi pia kwa nchi mbilli kupigana. Vita hii iliisha baada ya usuluhishi wa ataifa mengine na El savador ilifuzu kushiriki michuano ya kombe la dunia ambapo haikufanikiwa kuvukua hatua ya makundi.
  1. VITA YA NGURUWE(PIG WAR)
Mwaka 1859, katika mpaka kati ya marekani na Canada mabayo ilikua chini ya utawala wa Uingereza katika kisiwa cha San Juan kulikua na uhasama mkubwa kati ya nchi hizo mbili kwasababu ya kugombania kipande cha aridhi. Wakati huo kuna mmarekani alie kua analima viazi (Lyman Cutlar) upande mmoja na upande wa pili aliekuepo muingereza mmoja liekua akifuga nguruwe (Charles Griffin). Nguruwe mmoja wa griffin alivuka mpaka akaenda kula viazi vya Curtlar, ambaye alipata hasira na kumpiga risasi yule nguruwe na kusababisha kifo chake cutlar alikua tayari kumlipa Griffin dollar 10 lakini yeye alitaka dollar 100, ndipo ugomvi ulipoanzia na pande zote mbili ziltangaza vita, lakini viongozi wa Washington waliaamuru wanajeshi wao wasishambulie mpaka upande pinzani watakapoanza hivyo askari hao walitukanan mpakani kwa miezi kazaa mpaka viongozi walipo suluhisha mgogoro.

No comments: