Aliyekuwa mchezaji wa zamani wa Chelsea akitokea Ac Milani George Weah amefanikiwa kushinda nafasi ya urais iliyoachwa wazi na aliyekuwa rais Mstaafu Eileen nchini Liberia kwa kuwabwanga washindani wenzake 19 waliokuwa wakiwania kiti hicho cha urais.

Pia alifanikiwa kuchezea Timu ya taifa ya Liberia kwa mechi
70 , Mwaka 1989, 1994 na 1995, alitajwa
kama Mchezaji bora wa mwaka wa Afrika (African Footballer of the Year), na
mnamo mwaka 1996, alitatwa kuwa mchezaji bora wa karne wa Afrika ( African
Player of the Century).
George Weah alijiingiza kwenye siasa na kufanikiwa
kugombania nafasi kubwa ya kisiasa ( nafasi ya urais) kwa mara ya kwanza mwaka
2005 ambapo alibwagwa na Ellen Johnson
Sirleaf katika duru ya pili ya uchaguzi. Mwaka 2011 aligombania kama mgombea
mwenza ( makamu wa rais) wa Winston Tubman's lakini hakufanikiwa , 2014
alifanikiwa kuchaguliwa kuwa seneta kupitia chama cha Congress for Democratic
Change (CDC).
BOFYA HAPA KUONA GEORGE WEAH AKISAKATA KABUMBU
BOFYA HAPA KUONA GEORGE WEAH AKISAKATA KABUMBU
No comments:
Post a Comment