Aliyekuwa mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusuf Manji amevuliwa nafasi ya udiwani wa kata ya Mbagala Kuu baada ya kushindwa kuhudhuria vikao kutokana na kukabiliwa na kesi Mahakama ya Kisutu.
Manji
amepoteza sifa ya kuwa Diwani wa Kata hiyo kutokana na kutohudhuria
vikao zaidi ya sita na vikao vya kamati vya maendeleo ya halmashauri ya
Temeke zaidi ya vitatu.
Hayo
yamesemwa leo na Meya wa Manispaa ya Temeke, Abdallah Chaurembo katika
mkutano na waandishi wa habari kuhusu kuvuliwa udiwani kwa kiongozi
huyo.
Meya
Chaurembo ameongeza kwa kusema kuwa amemwandikia barua Waziri wa
Tamisemi, George Simbachawene kuhusu suala hilo ili aweze kupanga
uchaguzi mwingine.
Manji
ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Quality Group anakabiliwa na kesi ya
zaidi ya mbili moja ikiwa ni matumizi ya dawa za kulevya na nyingine
uhujumu uchumi.
Kwasasa
Manji yupo ndani kutokana na kesi hizo ambapo imepelekea mpaka
kushindwa kuhudhuria viako vya udiwani kwa ajili ya maendeleo ya kata
hiyo ya Mbagala Kuu jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment