Viongozi wanne wa Chama cha Wananchi CUF wanaomuunga mkono Profesa
Ibrahim Lipumba wamefariki dunia baada ya msafara wao kupata ajali
maeneo ya Ubenazomozi Mkoa wa Pwani.
Ajali hiyo imetokea jana usiku wakati Viongozi hao wakitokea Dodoma
kwenye sherehe za kuapishwa kwa Wabunge wapya wa Chama hicho.
Stori iliyonifikia asubuhi hii ya Jumatano September 6, 2017 ni kwamba
Viongozi wanne wa Chama cha Wananchi CUF wanaomuunga mkono Profesa
Ibrahim Lipumba wamefariki dunia baada ya msafara wao kupata ajali
maeneo ya Ubenazomozi Mkoa wa Pwani.
Ajali hiyo imetokea jana usiku wakati Viongozi hao wakitokea Dodoma
kwenye sherehe za kuapishwa kwa Wabunge wapya wa Chama hicho baada ya
gari lao kugongana na Lori.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Habari wa CUF Abdallah Kambaya Viongozi
waliofariki ni kutoka Wilaya ya Muheza, Tanga ambapo miongoni mwao ni
Mgombea Udiwani wa Muheza Mjini, aliyefahmika kwa jina moja Uredi.
Aidha, idadi ya majeruhi haijajulikana ila ni hawazidi 10 na baadhi yao
wapo Hospital ya Tumbi huku akisema chanzo cha ajali hiyo ni gari la
wafuasi hao kugongana na lori.
No comments:
Post a Comment