Msanii wa kike wa muziki wa Pop nchini Misri ajulikanaye kwa
jina la, Shyma amejikuta mikononi mwa polisi Jumamosi ya wikiendi iliyopita
baada ya kuachia video ya wimbo wake mpya ujulikanao kwa jina la ‘ I
have Issues’ kwa kosa la kuonekana akila tunda aina ya ndizi kwenye
video hiyo kwa mbwembwe mbele ya wanaume.
Moja ya kipande cha video hiyo kikimuonesha Shyma akila
ndizi.
Mrembo huyo kwenye video hiyo ambayo ilipata views milioni
1.2 ndani ya masaa 14 kwenye mtandao wa YouTube alionekana akila ndizi kwa
mbwembwe mbele ya wanafunzi wake huku akichora namba ‘#69’ ubaoni kitu ambacho
kiliamsha hisia kali kwa wanaume nchini Misri.
Polisi wamesema wanamshikilia kwa kosa la kukiuka maadili ya
dini ya kiislamu na tamaduni za nchi ya Misri huku wakidai kutaka kumuhoji
kujua zaidi alimaanisha nini kufanya hivyo kwenye video hiyo.
Shyma ambaye jina lake kamili ni Shaimaa Ahmed baada ya
kuona anashambuliwa na mashabiki wake mtandaoni aliamua kutolea maelezo kupitia
ukurasa wake wa Facebook akieleza kuwa hakuwa na wazo kama watu walivyofikiria
na kuomba radhi.
Leo Jumatano Polisi mjini Cairo wamesema watatoa taarifa
rasmi baada ya kufanya nae mahojiano kwa siku mbili mfululizo (Jumatatu na
Jumanne).
Mwaka 2015 Densa mmoja nchini humo alihukumiwa kifungo cha
mwaka mmoja jela na faini kwa kosa la kucheza akiwa amevaa nguo fupi huku akikatika
viuno kwenye sakafu.
Tayari video hiyo imeshatolewa kwenye mtandao wa YouTube
lakini hapa chini unaweza ukaangalia baadhi ya vipande ambavyo vimemuweka
rumande msanii huyo kama vilivyofanyiwa uchambuzi na Waandishi wa Habari.
ππππUNAWEZA ANGALIA KIPANDE πππππCHA VIDEO HIYO HAPA
No comments:
Post a Comment