MIKOA yote nchini imeagizwa kuwapima wananchi wake, virusi
vya ukimwi (HIV) bure kwenye wiki ya kuadhimisha Siku ya Ukimwi.
Wiki hiyo inaanza Novemba 24 na kuisha siku ya kilele cha
Siku ya Ukimwi duniani Desemba Mosi. Kaulimbiu ni “Changia mfuko, okoa maisha,
Tanzania bila Ukimwi inawezekana”. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,
Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama alisema hayo
jana.
Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu
maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yanayofanyika kitaifa Dar es Salaam.
Aliagiza kupatikana wataalamu wa kutosha kwa kila mkoa kwa upimaji huo na
ushauri nasaha.
Alisema katika wiki hiyo, kutazinduliwa Ripoti ya utafiti wa
kitaifa wa virusi vya Ukimwi, utafiti ambao hufanyika kila miaka minne. Alitaja
shughuli nyingine ni uzinduzi wa mkakati wa kondom wa kitaifa, kongamano la
kitaifa la wataalamu watakaojadiliana kukabili Ukimwi na huduma ya kupima kwa
hiari.
Chanzo-Habarileo
No comments:
Post a Comment