Habari zilizotufikia kutoka Kenya, Askofu Charles Okwany
ambaye baada ya kuichagua dini ya Kiislamu kuwa mwongozo wake wa wokovu duniani
na Akhera amechagua jina la Ismail Okwany.
Amesema amesilimu baada ya kufanya utafiti wa kina kuhusu
Uislamu. Amesema baada ya kusilimu, kanisa alilokuwa akihurbiri, lililoko
katika eneo la Nyalgosi kaunti ya Homa Bay magharibi mwak Kenya, ambalo
lilijulikana kwa jina la God’s Call Church of East Africa sasa limegeuzwa jina
na kuwa Msikiti wa Jamia wa Nyalgosi.
Katika mahojiano na Jarida la Nairobian, Ismail Okwany
amesema, wakati alipokuwa muhubiri wa Kikristo alikuwa akisafiri katika miji
mbali mbali ya Kenya na Tanzania hasa katika maeneo ya pwani na alipata fursa
ya kufanya utafiti kuhusu maisha ya Waislamu. Ismail Okwany anaongeza kuwa
aliweza kulinganisha Uislamu na Ukristo na akaamua kufuatia Uislamu.
Aidha anasema moja ya mambo yaliyokuwa yakimkera sana wakati
akiwa muhubiri wa Ukristo ni tabia ya wanawake kuingia ndani ya kanisa wakiwa
wamevaa sketi fupi katika hali ambayo wanawake Waislamu wanakuwa wamejisitiri
kwa Hijabu wakati wa ibada msikitini na hata nje ya msikiti.
Okwany mwenye umri wa miaka 65 alisilimu tarehe 26 Septemba
akiwa na wafuasi wengine 23 wa kanisa lake na sasa wako mbioni kusajili rasmi
msikiti wao.
Anasema Allaah (Subhanahu wa Ta’ala):
“Nyinyi ndio Ummah bora kuliko Ummah zote zilizodhihirishiwa
watu (ulimwenguni) mnaamrisha yaliyo mema na mnakataza yaliyo maovu, na
mnamuamini Allaah.” Aal ‘Imraan: 110
“Sema hii ndio njia yangu, ninaita (ninalingania) kwa Allaah
kwa ujuzi wa kweli, mimi (nafanya hivi) na (kila) wanaonifuata. Na Allaah
Ametakasika na kila upungufu, wala mimi simo miongoni mwa wanaomshirikisha
(Allaah).” Yuusuf: 108
CHANZO: JAMII FORUM
No comments:
Post a Comment