Takriban watu 15 wameuawa na
wengine 200 kujeruhiwa vibaya baada ya majeshi ya Israeli kulipua shule
inayoendeshwa na Umoja wa Mataifa kuwahifadhi wakimbizi wa ndani kwa
ndani wanaotoroka mashambulizi ya Isareli katika ukanda wa Gaza .
Wizara ya Afya katika ukanda wa Gaza
imedhibitisha shambulizi hilo katika shule hiyo iliyoko Beit Hanoun
ambayo inatumiwa kama makazi ya wakambizi wapalestina wanaotoroka
makombora ya Israili.Shambulizi hilo ni la nne kutokea katika vituo vinavyomilikiwa na Umoja wa Mataifa tangu Israeli ivamie ukanda huo yapata majuma mawili yaliyopita.
Kufikia sasa Wapalestina 725 wameuawa .
Israeli iliishambulia Gaza Julai tarehe 8 ikitafuta mbinu za kuzima mashambulizi ya makombora ya Hamas yanayotokea Gaza.
Awali mwsimamizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia maswala ya Misaada bi Valerie Amos alisema kuwa hali ya maisha imeendelea kuzorota katika ukanda huo na kuwa kuna haja ya dharura ya kusitishwa kwa vita ilikufanikisha utoaji wa misaada ya kibinadamu .
Bi Amos alisema kuwa watu laki moja (118,000) wanaishi katika kambi za umoja wa mataifa zilizoanzishwa katika shule zinazoendeshwa na UN.
Bi Amos amesema kuwa asilimia 44% ya Gaza hapakaliki kwa Wapalestina.
Hayo yamejiri baada ya Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu amesema kuwa anasikitikia vifo vya Wapalestina lakini wajibu unamtegemea kiongozi wa Hamas ambaye bado anashikilia kuwa Israeli hainabudi kukoma kuikalia Gaza kimabavu.
No comments:
Post a Comment