KINDA
wa muziki wa kizazi kipya nchini, Abdulaziz Abubakari ‘Dogo Janja’
amerejea tena jijini Dar es Salaam katika kundi la Tip Top Connection
baada ya kuwa mbali na kundi hilo kwa muda mrefu.
Dogo Janja aliondoka katika Tip Top mwaka 2012 na kuhamishia kazi
zake kwao Arusha baada ya kugombana na kiongozi wa kundi hilo, Ahmed
Ally ‘Madee’ aliyeonekana kama mbaya hadi kuamua kujiweka mbali na
msanii huyo.
Akizungumza na jijini Dar es Salaam, Madee alisema alikuwa amepanga
kumtaka Dogo Janja aombe radhi kupitia vyombo vya habari na akanushe
maneno aliyoyasema dhidi yake, lakini kwake ikawa ngumu.
“Dogo Janja alimuomba kwanza Mkubwa Fela na Babu Tale, wakaniambia
kuhusu kurejea Tip Top, nikawaambia kitu gani nataka azungumze na
waandishi kwa sababu hakuwahi kufanyiwa mambo aliyoyasema kwani
alichokuwa ametaka ni kuwa chini ya mtu mwingine.
Hata hivyo, Madee alisema baada ya kukaa na uongozi wa kundi waliona
kufanya hivyo itakuwa ni kudhalilishana tena, lakini pia Dogo Janja
alisema yote aliyoyasema ilitokana na umri wake kuwa mdogo.
Aliongeza kutokana na yeye kuwa mshika dini mzuri na huu ni mwezi
mtukufu, aliamua kumsamehe na kufungua ukurasa mpya wa maisha kwa
manufaa ya msanii huyo na tasnia ya muziki.
“Kwahiyo sasa hivi tuko naye Tip Top, hatutaki kuyaongelea yale
yaliyopita, tunataka tufunike kombe ili tuendelee na maisha mengine,”
alisema.
No comments:
Post a Comment