Monday, 14 July 2014

Mapigano bado yanaendelea Libya


Mapigano yazuka karibu na uwanja wa ndege wa Tripoli, Julai 13 mwaka 2014.
Mapigano yazuka karibu na uwanja wa ndege wa Tripoli,
Kumetokea mapigano kati ya wapiganaji hasimu jirani na uwanja wa ndege wa kimataifa mjini Tripoli nchini Libya. Waasi wanaopinga uislamu kutoka eneo la Zintan ambao wanadhibiti uwanja wa ndege wameshambuliwa na mahasimu wao waliokuwa wakijaribu kuteka eneo hilo.

Safari za Ndege kuingia na kutoka katika uwanja huo wa ndege zimesitishwa huku kukiwa na taarifa ya kusikika milipuko na milio ya risasi.
Wapiganaji wa Zintan wamekuwa wakipinga majaribio ya wapiganaji wa kiislamu kutwaa madaraka kwa nguvu tangu enzi za utawala wa Muammar Gaddafi mwaka 2011.
Serikali ya Libya imetolea wito pande husika katika mapiganio hayo kuanzisha mazungumzu, huku mataifa ya magharibi yakitiwa hofu na kuongezeka kwa machafuko nchini Libya. Marekani imeonya dhidi ya athari ambazo zinaweza kusambaa nchini nzima kutokana na mapigano hayo.
Kwa mujibu wa wizara ya afya, watu sita wameuawa na wengine 25 wamejeruhiwa katika mapigano ya jana.
Viongozi wa mamlaka ya uwanja ya ndege wameamua kufunga uwanja huo kwa muda wa siku tatu.
Uwanja huo wa ndege umeshambuliwa mapema asubuhi na wanamgambo amabo lengo lao ni kuwatimua waasi wa Zenten wanaopinga uislamu. Zenten ni mji unaiopatikana kusini magharibi mwa Tripoli.
Waasi hao wanashikilia uwanja wa ndege wa Zenten tangu kuangushwa utawala wa Kadhafi pamoja na maeneo mengine ya kijeshi yanayo unganisha barabara itokayo Tripoli kuelekea kwenye uwanja huo wa ndege.

No comments: