MSHAMBULIAJI Neymar amejaribu kuweka mambo sawa kuhusu tuzo ya Mpira wa Dhahabu aliyokabidhiwa Lionel Messi nchini Brazil.
Neymar amedai kwamba nahodha huyo wa Argentina "angalau" alikuwa miongoni mwa wachezaji watatu walioshika nafasi za juu kwenye Kombe la Dunia.
Messi aliiongoza nchi yake kutinga fainali mjini Rio de Janeiro, ambako walichapwa 1-0 na Ujerumani baada ya muda kuongezwa.
Neymar, ingawa, anaamini kwamba Messi, ambaye alishindwa kufunga katika hatua ya mtoano, alifanya vya kutosha nchini Brazil angalau kujiweka katika nafasi ya mgombea tuzo halali.
"Mimi ni shabiki mkubwa wa Messi, nikiwa kama mchezaji na kama mtu wa kawaida," yoso huyo wa Brazil alimzungumzia mchezaji mwenzake wa Barcelona wakati akihojiwa.
"Sijui kama ilikuwa halali au haikuwa halali kwa Messi kupewa tuzo, lakini kwangu mimi, alikuwa mmoja wa wachezaji katika Kombe la Dunia," alisema Neymar.
No comments:
Post a Comment