Sunday, 20 July 2014

Juhudi za kidiplomasia zaongezeka Gaza

Mashambulizi mapya ya jeshi la Israel yamesababisha vifo vya watu watano katika ukanda wa Gaza leo Jumapili na kupandisha idadi ya watu waliouwawa kutokana na mashambulizi hayo kufikia zaidi ya 350.
Ban Ki-Moon 17.06.2014 PK in Genf Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa
Wakati huo huo juhudi za kidiplomasia kuumaliza mzozo huo zinashika kasi wakati katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akitarajiwa kwenda katika eneo hilo.
Wakati Israel inaendelea na mashambulio yake ya anga, baharini na ardhini dhidi ya eneo hilo la pwani lililozingirwa, Hamas wanakataa kusalim amri, wakiendelea na mashambulio yao na kurejea madai ya kusitisha mapigano ya aina yoyote kufanyika.

Mkuu wa kundi la Hamas Khaled Meshaal alitarajiwa kukutana na rais wa Palestina Mahmud Abbas nchini Qatar kujadili pendekezo la Misri la kusitisha mapigano leo Jumapili, na kundi hilo limesema limepokea mwaliko kwenda Cairo kwa ajili ya mazungumzo ya kusitisha mapigano.
Hamas kwenda Cairo
Chaled Maschaal Hamas Chef
Mkuu wa Hamas Khaled Meshaal
Hamas "imepokea mwaliko, kupitia wapatanishi, kwa ajili ya ujumbe utakaoongozwa na Khaled Meshaal kuzuru Cairo na kujadili juhudi hizo za Misri," kundi hilo limesema katika taarifa.
Taarifa hiyo imesema kundi hilo la harakati zinazoongozwa na maelekezo ya dini ya Kiislamu "jibu lake kuhusiana na msimamo kuhusu juhudi hizo unafahamika, lakini wakati huo huo liko tayari kushirikiana na juhudi za upande wowote ambazo zitaafikiana na madai ya Wapalestina.
Katika siku ya 13 ya umwagikaji mkubwa wa damu katika mzozo wa Gaza katika miaka kadhaa, mashambulizi ya mapema alfajiri ya Israel katika mji wa kusini wa Rafah yamesababisha vifo vya watu watano, ikiwa ni pamoja na wanajeshi wawili katika shambulio la mtindo wa kikomandoo jana Jumamosi ndani ya ardhi ya Israel lililofanywa na wanamgambo wa Hamas.

Gazastreifen Bodenoffensive Israel 19.07.2014
Mashambulizi ya jeshi la Israel katika Gaza
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameondoka mjini New York jana Jumamosi na anatarajiwa kuwasili katika eneo hilo leo Jumapili kuimarisha juhudi za kidiplomasia zenye lengo la kumaliza umwagaji damu, ambao ni pamoja na idadi kubwa ya raia.
Israel inasema operesheni yake ina lengo la kumaliza kabisa mashambulizi ya maroketi ya wapiganaji yanayorushwa katika ardhi yake, na ghasia zimeongezeka tangu kuanzishwa kwa mashambulizi ya ardhini katika Gaza siku ya Alhamis.
Watoto wengi wauwawa
Gazastreifen Nahostkonflikt Bodenoffensive Soldaten
Wanajeshi wa Israel wakiingia Gaza
Miongoni mwa Wapalestina 47 waliouwawa jana Jumamosi, siku mbaya kabisa ya umwagikaji wa damu katika mzozo huo, ni watoto wawili wenye umri wa miaka sita na mtoto mchanga, amesema msemaji wa huduma za dharura Ashraf al-Audra.

Idadi kubwa ya watoto waliouwawa katika mzozo huo inasababisha malalamiko makubwa, wakati taarifa ya pamoja ya mashirika yasiyo ya kiserikali ya vita na ulinzi kwa watoto kimataifa ilisema watoto zaidi wameuwawa kuliko wapiganaji.
Idadi iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la UNICEF, inaonesha kuwa wahanga 73 ni watoto waliochini ya umri wa miaka 18.
Protest in Paris gegen Israels Kurs in Gaza 19.07.2014
Maandamano mjini Paris yakiunga mkono watu wa Gaza
Hamas hapo kabla wiki hii imekataa pendekezo la Misri la kusitisha mapigano, ambalo lilikubaliwa na Israel, ikisema kuwa haikushauriwa na kudai suluhisho kamili kabla ya kusitisha hatua ya kurusha makombora kutoka Gaza.

Afisa wa wizara ya mambo ya kigeni nchini Misri amesema hawezi kuthibitisha ama kukataa kuhusu mwaliko huo mpya.
Jeshi la Israel limesema leo kuwa linapanua mashambulio yake ya ardhini dhidi ya ukanda wa Gaza, ikiwa ni mzozo uliomwaga damu zaidi tangu mwaka 2009 ukiingia katika siku yake ya 13 na idadi ya watu waliouwawa ikivuka 350.

No comments: