Yanawezekana yakawa ni moja ya mauaji ya kutisha nchini, baada ya kijana mmoja kumuua mwanafunzi wa darasa la tatu Shule ya Msingi ya Marangu Hills Academy kisha kula ubongo wake.
Mbali na kula ubongo wa mtoto huyo, Francis Urassa
(9), mtuhumiwa huyo Lawrence Mramba alijikata sehemu za siri kwa
kutumia wembe na kuzila mithili ya mshikaki akikata kipande kimoja baada
ya kingine.
Hata hivyo, mtuhumiwa huyo naye alifariki dunia
saa chache baadaye baada ya kufikishwa Hospitali ya Kilema iliyopo Moshi
Vijijini wakati madaktari na wauguzi wakimpatia matibabu.
Mashuhuda wa tukio hilo lililotokea jana saa 1:00
asubuhi Kijiji cha Samanga, Wilaya ya Moshi Vijijini, walidai kijana
huyo alikuwa na nguvu za ajabu lakini baadae polisi walifanikiwa
kumdhibiti.
Mtuhumiwa Lawrence Mramba akila uume wake |
Lilikuwa ni tukio lililovuta hisia za wakazi wengi
waliokusanyika kijijini hapo huku wengine wakirekodi tukio la kijana
huyo kula uume wake kwa kutumia simu za mikononi.
Polisi kutoka Mji wa Himo walifika eneo la tukio
na kumkamata kijana huyo wakati huo akiwa katika hali mbaya kutokana na
kupigwa kwa mawe na wananchi na kujikata sehemu mbalimbali.
Mwili wa kijana huyo ulionekana ukiwa umetapakaa
damu kuanzia mdomoni hadi sehemu za siri kutokana na damu nyingi
kuchuruzika wakati akijikata uume vipande vipande na kuula.
RPC Kilimanjaro anena
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz
aliliambia bloger wetu jana kuwa chanzo cha tukio hilo ni upungufu wa
akili uliomkumba kijana huyo na kuanza kuvunja vioo vya nyumba.
“Leo (jana) asubuhi alimkata huyo mtoto wa tajiri
yake kwa panga na kisha na yeye akaanza kujikata sehemu zake za siri na
kula baadaye akajikata pia sehemu mbalimbali za mwili,” alisema.
Kwa mujibu wa Kamanda Boaz, mtuhumiwa huyo
alifariki katika Hospitali ya Kilema iliyopo Wilaya ya Moshi Vijijini
wakati madaktari na wauguzi wa hospitali hiyo wakimpatia matibabu.
Mtendaji wa kijiji asimulia
Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Samanga, Vick Lyimo
alisema siku moja kabla ya mauji hayo, kijana huyo aliyekuwa akijifunza
kazi ya Useremala alionekana kuchanganyikiwa kiakili.
Kutokana na kuchanganyikiwa huko, tajiri yake
aitwaye Fortunatus Urassa ambaye ni baba wa marehemu, alimchukua na
kumpeleka nyumbani kwake kwa ajili ya kupumzika.
Hata hivyo, mtendaji huyo alidai jana saa 1:00
asubuhi, wakati mtoto wa tajiri yake akitoka nyumbani kwenda shule
alimvamia na kumpasua kichwa kwa panga na kisha kula ubongo wake.
“Sasa baada ya kula huo ubongo ndio akaanza
kujitaka uume wake kipande kwa kipande na kukila mpaka polisi walipofika
kwa vile alikuwa akitishia watu kwa panga,” alisema mtendaji huyo.
Mchungaji wake ashikwa na butwaa
Mchungaji Ebeneza Ngomuo wa Kanisa la Pentecoste
Marangu alikokuwa akisali mtuhumiwa alisema haamini kilichotokea kwa
vile muumini wake huyo alikuwa ni mtu mpole na mtaratibu.
“Ni tukio la kusikitisha na siamini kama huyu
kijana yuko sawasawa kwa vile kabla ya tukio alikuwa anaonekana mara
zote ni mpole, mtaratibu na asiyetumia kilevi,” alisema mchungaji huyo.
“Sisi kama kanisa tumepata mshangao lakini naamini
huu ni mpango wa shetani kwa hali ya kawaida kijana huyo hawezi kufanya
unyama huu,” aliongeza mchungaji huyo na kusema;
“Siyo jambo rahisi mtu kula nyama ya binadamu
mwenzie na yeye mwenyewe kula nyama zake zikiwamo sehemu za siri...
lilikuwa ni tukio baya sana kuliona.”
Mtoto aliyeuawa alikuwa na uwezo kwenye masomo
Mwalimu wa Shule ya Marangu Hills Academy
alikokuwa akisoma mtoto Francis, Thomas Malulu alisema tukio hilo ni la
uchungu na limewaumiza sana wao kama familia ya shule hiyo
“Tukio hili ni la uchungu sana kwetu na familia ya Francis.
Alikuwa ni mtoto mwenye kipaji darasani na kwa kweli tukio hili limezima
ndoto yake,”alisema mwalimu huyo.
Mwalimu huyo alisema tukio hilo limeacha
kumbukumbu ambayo itawachukua muda mrefu kuwatoka na kusisitiza kuwa wao
kama wanadamu hawana la kufanya zaidi ya kumwachia Mungu.
No comments:
Post a Comment