Shirika la ndege la Taifa la Algeria, limesema
limepoteza mawasiliano na moja kati ya ndege zake iliyokua ikitoka
Burkinafaso kwenda Algiers kupita sahara.
Mawasiliano yalipotea dakika 50 baada ya ndege hiyo kupaa kutoka mji wa Ouagadougou, shirika hilo limeeleza.Chanzo cha habari kimeliambia shirika la habari la Ufaransa kuwa Ndege hiyo haikua mbali na mpaka wa Algeria wafanyakazi wa ndege hiyo walipoambiwa wabadili uelekeo kwa kuwa mawasiliano yalikua hafifu na kuepuka hatari ya kugongana na ndege nyingine katika njia ya Algiers-Bamako.
Mawasiliano yalipotea baada ya kubadilishwa kwa njia.
Ndege namba AH 5017 husafiri kupitia njia ya Ouagadougou-Algiers mara nne kwa wiki,AFP imeripoti.
Raia wa Algeria ni miongoni mwa abiria waliokuwa ndani ya Ndege hiyo,Gazeti moja la Algeria limeripoti.
No comments:
Post a Comment