Imearifiwa kua katika Mapigano yaliyozuka mpakani mwa Jamhurin ya
Kidemokrasia ya Kongo na Jamhuri ya Afrika ya Kati baina ya wanachama wa
Seleka na wanamgambo wa jeshi la Uganda watu 13 walipoteza maisha.
Katika maelezo yake msemaji wa jeshi la Seleka, Goma Narkoyo alisema
“siku iliyopita, palitokea mapigano baina ya askari wa Uganda na askari
wa Seleka kutokana na kutoelewana na kusababisha askari 1 na wanachama 2
wa Seleka kufariki.
“Kiongozi wa jeshi la UpinzanI, Joseph Kony
anatafutwa kwa visingizio vya ulinzi kwa ajili ya Uganda, Narkoy alisema
“ kwa miaka 6 sasa wanamsaka Kony hata hivyo hawajapata chochote. Wao
wanafanya biashara za dhahabu, pembe za ndovu na mbao. Wameshindwa
kusimamia majukumu yao, nasi tunataka waondoke”.
Msemaji wa jeshi la Uganda, Yarbay paddy Ankunda alisema mwanajeshi
mmoja aliwaua wanachama 11 wa Selek ana kuchukua silaha walizokuwa nazo.
Kumekua na ugomvi wa muda mrefu baina ya Jeshi la upinzani la Bwana na Uganda.
No comments:
Post a Comment