Saturday 19 July 2014

Wafanya kazi watatu katika mashirika ya misaada Darfur waachiliwa huru


Askari wa kuweka amani wa UNAMID Darfur
Maafisa wa kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kuweka amani Darfur, Sudan, wanasema kuwa wafanya kazi za misaada watatu waliotekwa nyara zaidi ya mwezi uliopita, wameachiliwa huru.
Kikosi cha Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa, UNAMID, walisema kuwa wanaume hao watatu - wote raia wa Sudan - walikuwa mateka wa mwisho kati ya watu 25 waliotekwa nyara mwezi uliopita huko Darfur kaskazini.
Waliobaki wameshaachiliwa huru.
Haijulikani nani aliwateka.
Ni kawaida kwa wafanya kazi wa mashirika ya misaada kukamatwa huko Darfur, eneo ambalo limekumbwa na mizozo katika miaka 11 iliyopita.

No comments: