Mzee Sumaye |
Sumaye aliyasema hayo mjini Arusha jana alipokuwa
akifungua mkutano mkuu wa Dayosisi ya Arusha, uliofanyika kwenye Ukumbi
wa Sekondari ya Peace House.
“Tanzania hatuna tatizo kubwa katika hili, lakini
hatuko salama sana. Kuna chokochoko za hapa na pale zinazoendelea zenye
sura ya kiimani. Hii ni ishara ya kuwa upendo, amani na mshikamano
miongoni mwetu umepungua na kuathiri umoja wetu.
“Tukiwa wamoja, sekeseke hili halitakuwa na nafasi
kwetu kwa sababu hakuna dini inayofundisha chuki wala kupigana, lazima
tuwe makini licha ya kila mtu kuwa na uhuru wa kuabudu bila kuvunja
sheria,” alisema Sumaye.
Alitoa wito kwa viongozi wa dini kuwasimamia vyema
waumini wao ili nchi isije ikakumbwa na balaa la vurugu za kidini,
jambo ambalo alisema ni la hatari kwa usalama wa nchi na watu wake.
Alisema wakati dunia inapita katika mapito
mbalimbali ya hatari, Watanzania hawana budi kung’ang’ania amani na
upendo walionao kwa masilahi ya ustawi wa jamii yao.
Alisema kuna nchi nyingi duniani ambazo zimeingia
katika migogoro iliyosababishwa na chuki za kidini na zimeishia katika
vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Aliwataka Watanzania katu wasikubali kuruhusu hali
hiyo itokee, bali waendeleze misingi ya amani, upande na utulivu
vilivyoachwa na waasisi wa taifa, akiwemo Baba wa Taifa, Mwalimu Julius
Nyerere.
No comments:
Post a Comment