Rais
Xi Jinping wa China amekutana na rais Mulatu Teshome wa Ethiopia katika
jumba la mikutano ya umma mjini Beijing. Kwenye mkutano wao Rais Xi
Jinping amesema China na Ethiopia zinaungana mikono na kusaidiana, na
uhusiano kati ya nchi mbili ni mzuri, na ni mfano wa kuigwa kati ya
China na nchi za Afrika, na kati ya nchi zinazoendelea. Amesema China
inaungana mkono kithabiti na Ethiopia katika juhudi zake za kustawisha
taifa, na inapenda kubadilishana uzoefu na Ethiopia kuhusu utawala na na
kuimarisha ushirikiano katika pande mbalimbali..
Rais Mulatu amesema Ethiopia na China zinaelewana na kuaminiana kwa
muda mrefu, serikali na wananchi wa Ethiopia wanaishukuru China kwa
uungaji mkono na misaada inayotoa kwa miaka mingi. Sasa wakati Ethiopia
inapohimiza maendeleo ya uchumi, inapenda kuiga uzoefu wa China. Pia
amesema Ethiopia inaukaribisha uwekezaji wa China, na inapenda kupanua
ushirikiano wa nchi hizo katika sekta za kilimo, utengenezaji na ujenzi
wa miundombinu..
No comments:
Post a Comment