Viongozi wa kieneo wanaosimamia upatanishi wa mgogoro wa Sudan
Kusini, wamezitaka pande hasimu nchini humo kufanya mazungumzo haraka
kwa lengo la kuikwamua nchi hiyo na mzozo wa ndani. Aidha viongozi hao
wameonya kuwa, ikiwa mazungumzo hayo hayatafanikiwa, basi nchi hiyo
changa zaidi barani Afrika, itarajie kukumbwa na matokeo mabaya. Hayo ni
kwa mujibu wa matamshi ya jana ya Hailemariam Desalegn, Waziri Mkuu wa
Ethiopia aliyeongeza kuwa, kila mazungumzo huwa yana ukomo na ni lazima
yafikie mwisho. Desalegn ameisitiza kuwa, nchi za eneo hilo hazipo
tayari kuona mazungumzo ya Sudan Kusini yakiendelea bila natija huku
raia wa nchi hiyo wakizidi kuteseka. Amezitaka pande hasimu kuwafikiria
kwanza wananchi wao badala ya kulinda maslahi yao binafsi. Amesema kuwa,
nchi za eneo hilo zinatoa tena fursa kwa mahasimu wa Sudan Kusini
kuhakikisha wanaelewana, na ikiwa hayo hayatafikiwa basi nchi hizo
hazitakuwa tayari kunyamanzia mauaji dhidi ya raia.
No comments:
Post a Comment