Jeshi la Cameroon linasema kuwa
kundi la wapiganaji Waislamu la Nigeria, Boko Haram, limemteka nyara
mke wa mwanasiasa mashuhuri kaskazini mwa nchi.
Mke wa naibu waziri mkuu, Amadou Ali, na
msaidizi wake wa nyumbani, walitekwa katika mji wa Kolofata, karibu na
mpaka wa Nigeria.
Inaarifiwa kuwa mapigano baina ya Boko Haram na wanajeshi wa Cameroon yanaendelea.
Boko Haram imefanya mashambulio kadha kaskazini
mwa Cameroon; na Jumamosi wafuasi zaidi ya 20 wa Boko Haram walifungwa
nchini Cameroon baada ya kukutikana na hatia ya kupanga mashambulio.
No comments:
Post a Comment