Monday, 21 March 2016

Tetesi za Usajili barani Ulaya

Kocha wa zamani wa Leicester Nigel Pearson amepewa kipaumbele kuja kuchukua mikoba ya kocha wa Aston Villa Mfaransa Remi Garde anayetegemewa kutimuliwa siku za hivi karibuni. (Chanzo Daily Mail)
Shirikisho la soka nchini Uingereza (FA) linataka kujaribu kwa mara ya mwisho kumzuia mshambuliaji wa Arsenal Alex Iwobi, 19, kuchukua uraia wa Nigeria. (Chanzo Daily Mirror)
Mabingwa wa nchini Italia Juventus watajaribu kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Oliver Giroud, 29, mwishoni mwa msimu ikiwa watamkosa chaguo lao namba moja, Edison Cavani, 29, wa Paris St-Germain. (Chanzo Tuttosport kupitia Daily Express)

Wakala wa kiungo wa Napoli Jorginho, 24, amewaalika Arsenal kuja kuanza mazungumzo ya makubaliano juu ya uhamisho wa mchezaji wake mwishoni mwa msimu. (Chanzo Radio Crc kupitia Metro)
Liverpool wameiulizia klabu ya Hoffenheim kama wanaweza wakampata beki wa kati wa klabu hiyo Niklas Sule mwenye umri wa miaka 20. (Chanzo Sports Bild kupitia Daily Star)
Wachambuzi mbali mbali barani Ulaya wanasema kuna uwezekano mkubwa kiungo wa Manchester City Yaya Toure, 32, akachagua kujiunga na Liverpool ikiwa ataamua kujiunga na klabu nyingine ya Ligi kuu Uingereza. (Chanzo Metro)
Kocha wa Leicester Claudio Ranieri amepanga kuelekea jiji la Roma kuitembelea familia yake wakati wa mapumziko ya kitaifa ili kujizuia na presha juu ya mbio za Ubingwa nchini Uingereza. (Chanzo Sky Sports)
Golikipa wa Stoke Jack Butland, 23, amesema ameongeza mkataba mpya wa miaka mitano na klabu yake kwa sababu anaamini klabu hiyo itafuzu mashindano mbalimbali ya Ulaya hapo baadae. (Chanzo Telegraph)
Golikipa wa Burnley Tom Heaton, 29, anaweza akaitwa mara moja kwenye kikosi cha England kufuatia golikipa wa Manchester City Joe Hart kuwa majeruhi. (Chanzo Lancashire Telegraph)
Manchester United wanaonekana kutaka kuwapiga kikumbo Arsenal kwenye kumsajili kiungo wa Atletico Madrid Saul Niguez, 21, kwa dili la paundi millioni 31. (Chanzo Don Balon kupitia Daily Express)
Hata hivyo, klabu hiyo ya Old Trafford huenda ikamkosa golikipa wa Genoa Mattia Perin, 23, ambaye wakala wake amesema mchezaji wake raia wa Italy anapenda kuendelea kubakia Seria A. (Chanzo Radio Kiss Kiss kupitia Daily Star)
Hizi ni baadhi ya habari tulizozipata siku ya leo, habari nyingine tukutane kesho panapo majaaliwa. LIKE page yetu ya “Spotibez” ili usipitwe na habari mpya za soka kutoka Ligi mbalimbali barani Ulaya na hapa Bongo

No comments: