Friday, 4 March 2016

Aliyesema hakuna Mungu nchin Urusi ashitakiwa

KrasnovAkipatikana na hatia, Krasnov huenda akafungwa jela mwaka mmoja
Mwanamume aliyeandika kwamba hakuna Mungu katika majibizano mtandaoni ameshtakiwa kusini mwa Urusi.
Viktor Krasnov aliripotiwa kwa polisi na wanaume wawili waliokasirishwa na lugha aliyoitumia wakati wa majibizano katika mtandao wa kijamii wa Kirusi wa VKontakte mwaka 2014.
Mtandao huyo hufanana sana na Facebook na ni maarufu sana.
Ameshtakiwa Stavropol kwa kosa la "kutusi hisia za waumini”.
"Matusi” kama hayo yaliharamishwa kisheria mwaka 2013 baada ya kesi ya Pussy Riot.
Wakati wa majibizano hayo, Bw Krasnov anadaiwa pia kupuuzilia mbali Biblia na kusema ni “mkusanyiko wa hadithi za kubuni za Wayahudi”.

Wataalamu wa lugha waliunga mkono msimamo wa Bw Krasnov kwamba maandishi yake yalikuwa “matusi kwa waumini” hao.
Kwa mujibu wa sheria ya Urusi, akipatikana na hatia, anaweza kufungwa jela mwaka mmoja na kutozwa faini ya hadi $4,083) au kufanyishwa kazi ngumu saa 240.

No comments: